Ibn ´Uthaymiyn kupangusa uso baada ya du´aa

Swali: Naomba kuwekewa  wazi juu ya jambo hili ambalo limenitatiza mimi na baadhi ya watu wengine. Ni ipi hukumu ya kudumu au kukithirisha kufuta uso kwa mikono miwili baada ya kumaliza kuomba du´aa? Khaswa ukizingatia ya kwamba baadhi ya watu wanatumia hoja kwa Hadiyth iliyotajwa na Ibn Hajar (Rahimahu Allaah) katika “Buluugh-ul-Maraam”?

Jibu: Kupangusa uso kwa mikono miwili baada ya kumaliza kuomba du´aa wapo wanachuoni wenye kuona kuwa kitendo hicho ni Bid´ah. Miongoni mwa walioona hivo ni Shaykh-ul-Islaam Ibn Taymiyyah (Rahimahu Allaah) na akasema kwamba Hadiyth zilizopokelewa kuhusu jambo hilo ni dhaifu na wala haziungani baadhi kwa zengine. Wanachuoni wengine wameona kwamba Hadiyth zilizopokelewa kuhusu hilo zikikusanywa zote zinafikia kiwango cha Hadiyth nzuri ambayo inafaa kutendewa kazi. Jambo hili pana. Mwenye kupangusa uso wake hakuna neno juu yake na mwenye kuacha kufanya hivo ndio bora zaidi.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Liqaa’ ash-Shahriy (59) http://binothaimeen.net/content/1343
  • Imechapishwa: 19/11/2019