Ibn ´Uthaymiyn kuongea wakati wa Khutbah ya ´Iyd

Swali: Ni ipi hukumu ya kuongea wakati wa Khutbah ya ´Iyd?

Jibu: Jambo hili wanachuoni wametofautiana. Wapo ambao wamesema ni haramu kuzungumza wakati imamu anakhutubu siku ya ´Iyd. Wapo wengine wamesema kuwa hakuna neno kwa sababu kuhudhuria sio wajibu. Hivyo kusikiliza pia sio wajibu.

Hapana shaka kwamba katika adabu ni mtu asiongee. Kwa sababu akiongea anaishughulisha nafsi yake, anawashughulisha vilevile wale wengine wanaozungumzishwa au ambao wanamsikiliza na kumtazama.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (16/247)
  • Imechapishwa: 14/06/2018