Ibn ´Uthaymiyn kuoa mwanamke anayeonyesha uso     

Swali: Ni ipi hukumu ya kuoa mwanamke asiefunika uso wake na atafunika baada ya kuolewa?

Jibu: Ni wajibu kwa msichana huyu kumcha Allaah (´Azza wa Jall) juu ya nafsi yake na juu ya wasichana wenzake wa rika lake. Asipojisitiri atakuwa ni ufunguo wa shari na atakuwa ni mwenye kuingia katika wale ambao Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema juu yao:

“Atayehuisha katika Uislamu msingi mbaya, atapata dhambi zake na dhambi za wataomuiga mpaka siku ya Qiyaamah.”

Lililo la wajibu juu ya mlezi wake ni kumkemea kutoka kwenda masokoni hali ya kuwa anaonesha uso wake au mwenye kuonesha mapambo.

Mwanamke akiona mlezi wake ni mtu wa msimamo kwelikweli, hunyenyekea na kumtii. Upande mwingine akiona kuwa ni mwenye kuchukulia wepesi, basi hufanya alitakalo.

Kuhusu kumchumbia msichana huyu, hakika Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) anasema:

“Mwanamke anaolewa kwa mambo mane; kwa mali yake, ukoo wake, uzuri wake na dini yake. Mchague yule mwenye dini mikono yako ifunikwe na mchanga.”

Haina shaka kuwa mwanamke anayeonesha mapambo na anatoka kwenda masokoni hali ya kuwa ni mwenye kuonesha mapambo, dini yake ni pungufu. Kwa hiyo achague mwanamke ambaye ni bora kuliko huyu.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Liqaa’ ash-Shahriy (11)
  • Imechapishwa: 03/05/2020