Ibn ´Uthaymiyn kuipwekesha ijumaa na jumamosi kwa kufunga sunnah

Swali: Je, inajuzu kupwekesha siku ya ijumaa katika kufunga swawm ya siku sita za Shawwaal?

Jibu: Ikiwa mtu amefunga siku ya ijumaa kwa sababu ndio siku ambayo yuko na nafasi na kuna uzito kwake kufunga siku nyingine isiyokuwa ya ijumaa ni sawa akafunga. Kwa sababu hakuifanya siku ya ijumaa kuwa ni maalum kwa sababu ni siku ya ijumaa. Ameifunga kwa sababu ndio siku ambayo yuko na nafasi. Ama akiifanya kuwa ni siku maalum pasi na sababu, tunamwambia ima aifunge pamoja na siku ya kabla yake au pamoja na siku ya baada yake. Vilevile inahusiana na siku ya jumamosi hafai kwake akaifanya kuwa ni maalu kwa kufunga. Anatakiwa ima aifunge pamoja na siku ya kabla yake au pamoja na siku ya baada yake. Vinginevyo asiifunge. Isipokuwa tu ikiwa kama atasema kuwa hana siku nyingine ambayo yuko na nafasi zaidi ya siku hii na kwamba anatamani kufunga siku hizi sita. Katika hali hii ni sawa. Kwa sababu hapo utakuwa hukuifanya kuwa ni maalum kwa sababu ni siku ya jumamosi.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Liqaa’ ash-Shahriy (17)
  • Imechapishwa: 19/11/2017