Ibn ´Uthaymiyn kuhusu wale wanaopinga kufunga masiku kumi ya Dhul-Hijjah

Swali: Kuna mwanamke mtumzima alikuwa na mazowea ya kufunga siku kumi za Dhul-Hijjah. Lakini mwaka huu kuna mtu alimjia na kumwambia haikuwekwa katika Shari´ah kufunga masiku haya kumi kwa sababu sio katika Sunnah kufunga masiku yote haya kumi na kwamba afunge masiku kumi mengine kama masiku meupe na siku ya ´Arafah. Anakuuliza juu ya hilo na anataka kutoka kwako umbainishie jambo lake kwa ufafanuzi.

Jibu: Ufafanuzi ni kuwa afunge masiku haya kumi midhali ni muweza na hilo halimtii uzito. Kwa kuwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Hakuna masiku yoyote matendo mema ndani yake yanapendwa zaidi na Allaah kama  masiku haya kumi.” Wakamuuliza: “Hata kupigana Jihaad katika njia ya Allaah?” Akasema: “Hata kupigana Jihaad katika njia ya Allaah. Isipokuwa mtu ambaye ametoka na nafsi yake na mali yake na asirudi na chochote katika hayo.”

Tunamuuliza: je, kufunga hakuingii katika matendo mema? Jibu ni ndio. Ndio maana Allaah ameifanya ni katika nguzo za Uislamu. Hapana shaka ya kwamba kufunga kunaingia katika matendo mema. Allaah (Ta´ala) amesema katika Hadiyth ya kiungu:

“Swawm ni Yangu na mimi ndiye nitailipa.”

Mambo yakiwa hivo basi tunasema kuwa swawm imewekwa katika Shari´ah. Mwenye kudai kwamba haitakiwi kufunga basi alete dalili inayotoa swawm katika ujumla huu:

“Hakuna masiku yoyote matendo mema ndani yake yanapendwa zaidi na Allaah kama  masiku haya kumi.”

Endapo itathibiti kuwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) hakuyafunga, hili ni jambo la kibinafsi. Huenda alikuwa hayafungi kwa sababu alikuwa ni mwenye kujishughulisha na mambo yaliyo na manufaa na muhimu zaidi. Lakini hata hivyo sisi tuna tamko la Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

“Hakuna masiku yoyote matendo mema ndani yake yanapendwa zaidi na Allaah kama  masiku haya kumi.”

Pamoja na kuwa imepokelewa kutoka kwake ya kwamba (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alikuwa haachi kuyafunga. Imaam Ahmad ametanguliza hili, ya kwamba alikuwa haachi kuyafunga, juu ya upokezi unaopinga na akasema:

“Mwenye kuthibitisha anatangulizwa kabla ya mwenye kupinga.”

Lakini hata tukisema kwamba hakuna dalili inayofahamisha kuwa alikuwa akifunga inaingia katika ujumla:

“Hakuna masiku yoyote matendo mema ndani yake yanapendwa zaidi na Allaah kama  masiku haya kumi.”

Kuhusu kufunga masiku meupe mtu hawezi kuyafunga katika Dhul-Hijjah. Kwa sababu siku ya tarehe kumi na tatu ni katika yale masiku ya kuchinja ambayo ni haramu kufunga.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Liqaa’ ash-Shahriy (34) http://binothaimeen.net/content/749
  • Imechapishwa: 26/11/2017