Ibn ´Uthaymiyn kuhusu vitabu vya dini vilivyo na picha

Swali: Je, ni lazima kwa mtu kuharibu picha ilio kwenye kitabu? Je, kuweka msitari kati ya shingo na kiwiliwili kunaondosha uharamu?

Jibu: Sioni kuwa ni lazima kuiharibu. Kwa sababu katika kufanya hivo kuna uzito mkubwa. Jengine ni kwamba vitabu hivi havikukusudia picha hii. Wamekusudia mafunzo yaliyomo ndani yake. Kupiga mstari kati ya shingo na kiwiliwili hakubadilishi picha kama ilivyo.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (02/283)
  • Imechapishwa: 03/07/2017