Swali: Je, kuacha kuswali Tahiyyat-ul-Masjid imechukizwa? Je, ni wajibu kwangu kumuamrisha yule mwenye kuacha kuswali Tahiyyat-ul-Masjid kuswali Rak´ah mbili?

Jibu: Kuacha kuswali Tahiyyat-ul-Masjid imechukizwa kwa maono ya baadhi ya wale  wanachuoni wenye kuonelea kuwa Tahiyyat-ul-Masjid ni wajibu. Maoni haya ni yenye nguvu sana. Yana mtazamo. Kwa sababu kuna mtu aliingia msikitini siku ya ijumaa wakati Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alipokuwa akiwakhutubia watu ambapo mtu yule akakaa. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akamuuliza:

“Je, umeshaswali?” Akajibu: “Hapana.” Akamwambia: “Simama na uswali Rak´ah mbili na uzikhafifishe.”

Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alikatiza Khutbah yake kwa ajili ya kuzungumza na mtu huyu. Isitoshe (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akamwamrisha vilevile kuswali pamoja na kuwa wakati yuko anaswali kutamshughulisha na kusikiliza Khutbah. Ni jambo lenye kujulikana kwamba kusikiliza Khutbah ni wajibu. Wamesema wale wenye kuonelea kuwa Tahiyyat-ul-Masjid wametumia hoja kwa kusema:

“Hakuna kitu kitachoshughulisha kutokamana na wajibu isipokuwa jambo la wajibu lingine.”

Kwa hivyo ukimuona mtu ameingia msikitini na akakaa, basi unatakiwa kumuuliza kama ameshaswali. Akisema kuwa amefanya ni sawa.  Akisema kuwa hana twahara ni sawa. Kwa sababu huwezi kumwambia aswali ilihali hana wudhuu´. Lakini endapo atasema kuwa yuko na wudhuu´ na hajaswali, basi unatakiwa kumwambia asimame na aswali Rak´ah mbili. Fanya hivo ili usije kuingia kwenye madhambi. Kwa sababu wale wenye kuonelea kuwa swalah ya Tahiyyat-ul-Masjid ni wajibu wanaona kuwa iwapo mtu ataiacha basi anapata dhambi.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Liqaa’ ash-Shahriy (35) http://binothaimeen.net/content/782
  • Imechapishwa: 17/01/2018