Swali: Ni ipi hukumu ya kupiga kura Kuwait khaswa kwa kuzingatia kwamba waislamu wengi na wanamme wanaolingania katika Uislamu wamepewa mtihani. Ni ipi hukumu ya ujaziaji kura huko Kuwait?

Jibu: Mimi naona kuwa upigaji kura ni lazima. Lazima tuwasaidie wale ambao tunawaona kuwa ni wema. Vinginevyo ni kina nani wataochukua sehemu za watu hawa wema? Hapana shaka kwamba ima ni wale waovu au watu wasiokuwa wema wala waovu wanaomfuata kila mtu na kila kitu. Kwa hiyo ni lazima tumchague yule ambaye tunamuona kuwa ni mwema.

Pengine mtu akauliza:

”Tumemchagua mmoja, lakini bunge karibu zote ni mbaya.”

Hakuna neno. Huyu mmoja ikiwa Allaah ataweka baraka ndani yake na akazungumza neno la haki ndani ya bunge hili, basi hapana shaka kwamba litakuwa na athari juu ya bunge. Lakini tatizo ni kwamba hatuko wakweli pamoja na Allaah. Tunategemea mambo ya kilimwengu na tunapuuza maneno ya Allaah (´Azza wa Jall).

Unasemaje juu ya Muusa ambaye alitaka kuwapa changamoto wachawi mchana kweupe siku ya sikukuu na siku ya wazi yenye kuonekana? Watu wote wamekuja. Muusa (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akawaambia:

قَالَ لَهُم مُّوسَىٰ وَيْلَكُمْ لَا تَفْتَرُوا عَلَى اللَّـهِ كَذِبًا فَيُسْحِتَكُم بِعَذَابٍ ۖ وَقَدْ خَابَ مَنِ افْتَرَىٰ

”Akawaambia: ”Ole wenu! Msimzulie Allaah uongo akakufutilieni mbali kwa adhabu. Hakika atashindwa anayezua uongo.”[1]

Neno moja, lakini likawa zito kama bomu. Allaah (´Azza wa Jall) amesema:

فَتَنَازَعُوا أَمْرَهُم بَيْنَهُمْ وَأَسَرُّوا النَّجْوَىٰ

“Wakavutana jambo lao baina yao na wakanong’ona kwa siri.”[2]

Waliyasema haya baada ya maneno yake. Wakivutana watu juu ya jambo basi inajulisha kushindwa. Matokeo yake wachawi hawa ambao wamekuja kwa ajili ya kushindana na Muusa wakajiunga pamoja naye. Wakaenda chini wakimsujudia Allaah:

فَأُلْقِيَ السَّحَرَةُ سُجَّدًا قَالُوا آمَنَّا بِرَبِّ هَارُونَ وَمُوسَىٰ

“Wachawi wakaangushwa wanasujdu wakisema: “Tumemwamini Mola wa Haaruun na Muusa.”[3]

Fir´awn akiwa ni mwenye kusimama mbele yao. Neno moja lililotoka kwa mmoja likaathiri watu wengi mbele ya kiongozi. Hata kama tutajaalia kuwa bungeni hakuna isipokuwa watu wachache walioshikamana na haki na usawa, basi watatoa manufaa. Muhimu ni kwamba wanatakiwa kuwa wakweli kwa Allaah (´Azza wa Jall).

Wako wanaosema kuwa haijuzu kushiriki bungeni kwa sababu ni kushirikiana na kukaa na watenda madhambi. Je, sisi tumeketi nao kwa ajili ya kukubaliana nao? Tumeketi nao kwa ajili ya kuwabainishia haki. Baadhi ya wanachuoni wanasema kuwa haijuzu kwa mtu mwema kukaa na mtu aliyepinda. Je, mtu huyu mwema ameketi kando ya aliyepinda ili aweze kupinda au kurekebisha yaliyopinda? Amefanya hivo ili aweze kunyoosha kile kilichopinda. Ikiwa hatoweza kufanya hivo hivi sasa, basi ataweza kufanya hivo mara nyingine.

Swali: Ni uchaguzi wa ujaziaji kura.

Jibu: Hali kadhalika. Mpe kura yako yule ambaye unaona kuwa ni mwema na mtegemee Allaah.

[1] 20:61

[2] 20:62

[3] 20:70

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Liqaa’-ul-Baab al-Maftuuh (211)
  • Imechapishwa: 19/10/2020