Ibn ´Uthaymiyn Kuhusu Tawhiyd-ul-Haakimiyyah

Swali: Unasemaje kwa mwenye kusema kuwa kuna aina ya tatu ya Tawhiyd iitwayo Tawhiyd-ul-Haakimiyyah?

Jibu: Tunasema mtu huyu kapotea na ni mjinga. Kwa kuwa Tawhiyd-ul-Haakimiyyah ni Tawhiyd ya Allaah (´Azza wa Jall). Mwenye kuhukumu ni Allaah (´Azza wa Jall). Ukisema Tawhiyd imegawanyika mafungu matatu, kama walivyosema wanachuoni… Tawhiyd-ur-Rubuubiyyah, yaani Tawhiyd-ul-Haakimiyyah inaingia katika Tawhiyd-ur-Rubuubiyyah. Kwa kuwa Tawhiyd-ur-Rubuubiyyah ina maana ni Allaah peke Yake ndo Mwenye kuhukumu. Vilevile ni Allaah (´Azza wa Jall) ndiye Mwenye kuumba na kuendesha mambo yote. Kauli hii imezushwa na ni munkari. Na vipi Tawhiyd-ul-Haakimiyyah itakuwa yenyewe? Kauli hii imezushwa na ni munkari. Kama anamaanisha kuhukumu, mwenye kuhukumu ni Allaah peke Yake nayo inaingia katika Tawhiyd-ul-Haakimiyyah. Kwa kuwa Mola ndiye Mwenye kuumba, Mfalme na Mwenye kuendesha mambo yote. Hii ni Bid´ah na upotofu.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Liqaa’ al-Baab al-Maftuuh (150 A)
  • Imechapishwa: 16/10/2020