Swali: Je, Raafidhwah wote kwa ujumla wanafanyiwa Takfiyr?

Jibu: Raafidhwah ni kama Ahl-ul-Bid´ah wengine wote hawako katika daraja moja.Wanatofautiana sana. Kuna wanaokufuru. Na wengine sivyo hivyo. Na miongoni mwao kuna ´Awwaam wasiojua kitu. Mtu hawezi kuwapa hukumu ya kijumla mpaka aangalie kila mmoja binasfi. Na hali kadhalika Mu´tazilah, Jahmiyyah na wengineo katika Ahl-ul-Bid´ah.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Liqaa’ al-Baab al-Maftuuh (189 B)
  • Imechapishwa: 09/04/2022