Pete ya ndoa wanandoa huvishana wanapotaka kuoana au baada ya kuoana. Desturi hii haitambuliki kwetu hapo kabla. Shaykh al-Albaaniy (Waffaqahu Allaah) ametaja kwamba imechukuliwa kutoka kwa manaswara na kwamba mapadiri huwaletea mume na mke wanaotaka kufunga ndoa makanisani na mwanamke anavishwa pete ima kwenye kidole cha mwisho, kidole cha pete au kidole cha katikati. Sijui namna inavofanywa. Lakini anasema kwamba ni desturi iliyochukuliwa kutoka kwa manaswara[1]. Ni jambo lisilokuwa na shaka kwamba kuepuka jambo hilo ndio bora zaidi ili tusije kujifananishe na wasiokuwa sisi.

Naongezea juu ya hilo kwamba wako baadhi ya watu ambao wanaitakidi juu ya hilo imani fulani ambapo wanaandika jina la mwanaume yule ambaye anataka kumpa pete ile ambapo na mwanamke anafanya hali kadhalika. Wanaamini muda wa kuwa pete bado iko mikononi mwao na ina majina yao basi hawatotengana. Imani hii ni aina ya shirki. Ni miongoni mwa Tiwalah ambayo wanadai kwamba inampendekeza mwanamke kwa mume wake na mume kwa mke wake. Kukiwepo imani hii ni haramu. Kwa hiyo pete katika hali hii inakuwa imeambatana na mambo mawili:

Mosi: Imechukuliwa kutoka kwa manaswara.

Pili: Mume akiamini kwamba ni sababu inayopelekea kuwafungamanisha kati yake yeye na mke wake, basi inakuwa ni aina ya shirki. Kujengea juu ya hili tunaona kuwa kuiacha ni bora zaidi.

[1] Tazama https://firqatunnajia.com/46-maovu-ya-sita-pete-ya-uchumba/

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Liqaa’ ash-Shahriy (46) http://binothaimeen.net/content/1055
  • Imechapishwa: 09/03/2019