Ibn ´Uthaymiyn kuhusu mwanamke kutumia baruka

Swali: Inajuzu kwa mwanamke kutumia baruka?

Jibu: Baruka ni haramu na linaingia katika kuunganisha nywele. Hata kama sio kuunganisha moja kwa moja baruka linaonyesha kichwa cha mwanamke kwa njia ya urefu inayofanana na kuunganisha. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amemlaani mwenye kuunganisha nywele na yule mwenye kuunganishwa.

Lakini ikiwa mwanamke kichwani hana nywele kabisa hakuna ubaya akatumia baruka hili kwa ajili ya kuficha aibu hii. Kwa sababu kuficha aibu ni jambo linalojuzu. Kwa ajili hiyo ndio maana Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alimpa idhini mtu mmoja ambaye pua yake ilikatika katika moja ya vita na badala yake atumie pua ya dhahabu. Masuala ni mapana kuliko hivo.  Ndani yake kunaingia masuala ya kujipamba na upasuaji. Ikiwa ni kuondosha aibu hakuna neno. Ni kama mfano mtu akawa na pua lililopinda ambapo akaliweka sawa au akaondosha mahali paliposhika weusi. Mfano wa haya hakuna ubaya. Lakini ikiwa sio kwa lengo la kuondosha aibu kama mfano wa kutia mwanya kati ya meno na kunyoa nyusi. Haya ndio yaliyokatazwa.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (11/137)
  • Imechapishwa: 30/06/2017