Ibn ´Uthaymiyn kuhusu mswaliji kuinuka kabla ya Tasliym ya pili ya imamu

Swali: Ambaye alikuja amechelewa kuingia katika swalah akiinuka katika swalah baada ya Tasliym ya imamu ya kwanza na kabla ya Tasliym ya pili swalah yake inabatilika?

Jibu: Swalah yake sio batili. Lakini kuna baadhi ya wanachuoni wamesema katika hali hii swalah yake inageuka kuwa swalah ya sunnah na haizingatiwi kwake kuwa ni ya faradhi. Hivyo ni kwa sababu amejitenga na imamu kabla ya kutimia swalah ya imamu. Kwa sababu swalah ya imamu haimaliziki isipokuwa baada ya Tasliym ya pili. Pindi ataposimama kukidhi yaliyompita basi amejitenga kabla ya swalah ya imamu wake. Wamesema kuwa inageuka kuwa ya sunnah. Kwa sababu swalah ya sunnah kwa mtazamo wa wengi katika watu hawa wanaonelea kuwa mtu anaweza kutoka kwa Tasliym moja.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Liqaa’ ash-Shahriy (37) http://binothaimeen.net/content/826
  • Imechapishwa: 14/03/2018