Ibn ´Uthaymiyn kuhusu mfungaji kutumia dawa za matone machoni, masikioni na puani

Swali: Nimesikia katika moja ya darsa zako ukisema  ya kwamba tone halifunguzi hata kama litafika kwenye korome kwa sababu haina maana ya kula na kunywa. Ama moshi hautakiwi kuvutwa kwa pumzi kwa sababu una virutuba na kwamba ukifika katika koo unafunguza. Ni vipi moshi utafunguza ilihali hayo hayana maana ya kula na kunywa?

Jibu: Ama kuhusu tone kwenye macho au kwenye masikio ni mambo hayaharibu swawm ijapokuwa yatafika kwenye koo. Kwa sababu huku sio kula, kula wala hayana maana ya kula na kunywa. Isitoshe jengine ni kwamba macho na masikio sio viungo vilivyozoeleka vinavyofikisha chakula tumboni. Lakini kuvuta kitu kwa pumzi ni katika mambo yaliyozoeleka katika kufikisha kitu tumboni.  Dalili juu ya hilo ni kwamba Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alimwambia Qaytw bin Swabirah:

“Pitiliza katika kupalizia isipokuwa ikiwa umefunga.”

Hii ni dalili inayoonyesha ya kwamba chenye kuingia puani ni kama chenye kuingia kinywani. Hii ndio tofauti. Kwa ajili hii tunasema hakuna ubaya kwa mfungaji kujifukiza, mafuta, manukato ya harufu mbalimbali za kunukia na vinginevyo. Lakini asivute kwa pumzi ule moshi wa uvumba. Kwa sababu unaweza kufika tumboni mwake.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Liqaa’ ash-Shahriy (41) http://binothaimeen.net/content/1505
  • Imechapishwa: 13/06/2018