Ibn ´Uthaymiyn kuhusu mapinduzi ya Kiislamu


Swali: Baadhi ya waandishi wanatumia neno “mapinduzi”, “mapinduzi ya kiutume” na “mapinduzi ya Kiislamu”. Je, taabiri hii ni sahihi? Vipi kuwaraddi?

Jibu: Hapana si sahihi. Je, Allaah aliita kuwa ni “mapinduzi”? Au aliita kuwa ni “uongofu” na “haki”? Aliita kuwa ni uongofu na haki.

يَا أَيُّهَا النَّاسُ قَدْ جَاءكُمُ الرَّسُولُ بِالْحَقِّ

“Enyi Watu! Amekwisha kujieni Mtume huyu na haki itokayo kwa Mola Wenu.” (04:170)

Hakusema Mtume kafanya mapinduzi kwa masanamu. Tunawaraddi kwa hili. Hatuwezi kupindua uongofu, nuru na haki na kusema ni mapinduzi. Waambie watu katika mji wako hivi. Waambie ni haki, nuru, uongofu na dawa.

Swali: Je, kuna mapinduzi ya Kiislamu?

Jibu: Hakuna mapinduzi ya Kiislamu kamwe. Hata hivyo ni sawa kusema kwamba ni ongofu wa Kiislamu.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih Ibn ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Liqaa' al-Baab al-Maftuuh (204 B)
  • Imechapishwa: 06/09/2020