Ibn ´Uthaymiyn kuhusu kuwatahiri watoto

Swali: Muislamu katika jamii za waislamu, mbali na nchi hii, anafikwa na baadhi ya matatizo ya kijamii. Matokeo yake muislamu anakuwa ni mwenye kudangana kwa sababu ya dalili zenye kukidhi kiu na zenye kutosheleza kutokuwa wazi kwake. Miongoni mwa mambo yenye kunitatiza ni kwamba sisi tuko na watoto wa kike na sasa wamekuwa na miaka kumi na mpaka sasa bado hawajatahiriwa. Katika nchi yetu mwanamke akiwa bado hajatahiriwa basi hiyo inakuwa ni aibu anayoaibishwa nayo mwanamke na wanamsifu kwa mambo mabaya. Mimi niko katika jamii hii. Naomba uniwekee wazi mimi na wengi ambao ni mfano wangu na katika hali yangu na utupe fatwa ambayo itampa amani na utulivu muislamu. Je, kumtahiri mwanamke ni Sunnah kama tulivyosikia?

Jibu: Kutahiri au kukereketa, baadhi ya wanachuoni wamesema kuwa ni wajibu kwa mvulana na msichana.

Wanachuoni wengine wakasema kuwa ni Sunnah, na sio wajibu, kwa wavulana na wasichana.

Maoni ya tatu ndio ya katikati. Wamesema kuwa kutahiri ni wajibu kwa wavulana na ni Sunnah kwa wasichana. Haya ndio maoni ya kati na kati na ndio yanayofahamishwa na dalili za wazi zinazotegemewa. Kama anataka kuwatahiri ni sawa na wala hakuna dhambi juu yake midhali wasichana hao wamefikisha miaka kumi na mbili.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Liqaa’ ash-Shahriy (54) http://binothaimeen.net/content/1234
  • Imechapishwa: 17/09/2019