Ibn ´Uthaymiyn kuhusu kutoga masikio na pua

Swali: Ni ipi hukumu ya kutoga sikio au pua ya msichana kwa ajili ya mapambo?

Jibu: Sahihi ni kwamba kutoga sikio hakuna ubaya. Haya ni katika malengo ambayo kunafikiwa kwayo kufanya jambo lililoruhusiwa. Imethibiti ya kwamba wanawake wa Maswahabah walikuwa na vipuli wakivaa kwenye masikio yao. Hili ni jambo lepesi. Mtu anapotogwa utotoni kunapona haraka.

Kuhusu kutoga pua sikumbuki ni kipi wanachosema wanachuoni. Lakini mimi naona kuwa kunafanya mtu akaonekana vibaya maumbile yake na kuumbuka. Pengine kuna wengine wasiokuwa sisi wenye kuonelea kuwa haifai.

Ikiwa wanawake katika mji fulani wanachukulia kutogwa pua ni katika mapambo, basi itakuwa hakuna ubaya kutoga pua ili kuning´iniza kipini  juu yake.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (11/137)
  • Imechapishwa: 30/06/2017