Ibn ´Uthaymiyn kuhusu kutaja kosa la mtu ambaye anatahadharishwa 02


Swali: Mtu akitumbukia ndani ya Bid´ah au Bid´ah inayoweza kuwa ya khatari na nikaonelea kutaja kosa lake – ni lazima kutaja mazuri yake au ni lazima kutaja Bid´ah hiyo, kosa hilo peke yake, au ni lazima kwangu kufanya kitu kingine kama vile kutaja mazuri yake?

Jibu: Jawabu linahitaji upambanuzi. Mtu anayetaka kumthamini mtu na kutaja maisha yake, basi ni lazima kutaja mazuri na mabaya yake.

Ama ambaye anataka kunasihi na kutahadharisha Bid´ah na kosa lake, asitaje mazuri yake. Ukitaja mazuri yake hiyo ina maana kwamba unawavutia watu kwake. Kwa hivyo swali linahitaji upambanuzi.

Mtu akizua Bid´ah na wakati huohuo tunataka kutadharisha Bid´ah hiyo, tunamtaja mtu huyo. Hakuna neno katika hali hiyo. Hata hivyo kunaweza kuwepo manufaa makubwa kutomtaja kwa jina lake.

Lakini kama tunataka kuzungumzia maisha yake, basi ni lazima kutaja yale yaliyo upande wake na yaliyo dhidi yake. Kwa hivyo swali linahitajia upambanuzi.

Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) aliwataja baadhi ya watu kwa majina yao wakati ilipokuwa inahusiana na nasaha. Kama mfano wa Hadiyth ya Faatwimah bint Qays ambaye alisimulia kuwa Abu Jahl, Mu´aawiyah na Usaamah bin Zayd wamemchumbia. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akamtaja kwamba Abu Jahm na Mu´aawiyah kwa njia inayompelekea yeye kutoolewa nao. Badala yake akamwambia aolewe na Usaamah. Hakutaja mazuri yao ingawa mazuri yao hapana shaka kwamba ni mengi. Alinyamazia hilo kwa sababu nafasi inapelekea kufanya hivo. Lakini ikiwa mtu anataka kuzungumzia maisha ya mtu, basi ni lazima awe mwadilifu na kutaja yale yaliyo upande wake na yaliyo dhidi yake.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Liqaa' al-Baab al-Maftuuh (121 B) Tarehe: 1416-11-16/1996-04-04
  • Imechapishwa: 18/07/2021