Ibn ´Uthaymiyn kuhusu kusikiliza nyimbo

Swali: Hivi punde kumeenea khaswa kati vijana wakiume na wakike kusikiliza idhaa zinazorusha muziki. Idhaa hizo zimetenga redio ambazo ni maalum. Tunaona kuwa idadi kubwa ya vijana wamekuwa ni wenye kusikiliza hayo kwa wingi. Bali utawaona vijana njiani wanapaza sauti ya juu kabisa na wanazunguka kwenye mabarabara na sauti hiyo. Ni ipi nasaha zako?

Jibu: Kuhusu nasaha kwa watu wote lililo la wajibu ni kujiepusha na nyimbo hizi. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ameeleza kuwa watakuwepo katika Ummah wake watu ambao wanahalalisha uzinzi, hariri, pombe na ala za muziki. Mnajua nini uzinzi? Zinaa. Hivyo Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akaambatanisha uhalalishwa wa pombe, uzinzi na ala za nyimbo. Ala za nyimbo (المعازف) kwa mujibu wa lugha ya kiarabu na kwa wanachuoni ni nyenzo za pumbao. Nyimbo hizi zinazosikizwa hazijiepuki ala za pumbao. Kwa hivyo kuzihalalisha ni haramu. Kuzisikiliza ni haramu. Kuzinyanyua sauti kati ya waislamu ni haramu. Kwa hivyo ni wajibu kukomeka na hilo; zisikizwe na kanda zake zisirushwe ili tuwe Ummah mwema unaoshirikiana katika wema na uchaji na si kinyume chake.

Ifahamike kuwa hawa ambao wananyanyua sauti za nyimbo hizi ikiwa makusidio yao ni kuwatweza wanachuoni na watu wa dini, basi uhakika wa mambo ni kuwa hakuwatweza watu kutokana na utu wao. Amewatweza kwa sababu ya ile elimu ya Shari´ah waliobeba na dini ya Allaah (´Azza wa Jall). Hivyo basi yuko katika khatari kubwa kwa sababu Allaah anaweza kuupotosha moyo wake na akamuharibia dini na dunia yake. Upande mwingine ikiwa makusudio yake ni kwamba wasikize wale wanaopenda nyimbo ili aweze kuwavuta kwake, hili ni khafifu kidogo kuliko lile la mwanzo. Lakini hata hivyo pia ni baya.

Kwa hivyo ni wajibu kutahadhari na nyimbo hizi na mtu badala yake asikilize kanda za Qur-aan, kanda za Hadiyth au kanda za kielimu ili mtu aweze kufaidika.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Liqaa’ ash-Shahriy (38) http://binothaimeen.net/content/868
  • Imechapishwa: 01/07/2018