Ibn ´Uthaymiyn kuhusu kupiga kura

Swali: Umesema kuwa inafaa kupiga kura? Ni ipi hukumu ya hilo?

Jibu: Ndio, tumefanya hivo. Ni lazima watu wafanye hivo. Ikiwa kura za waislamu zitapotea, basi watu waovu pekee ndio watakaokaa bungeni.

Waislamu wakishiriki katika uchaguzi, wakawapigia kura wale ambao wanaona kuwa ni wastahiki. Basi kwa njia hiyo itafikiwa kheri na baraka.