Ibn ´Uthaymiyn kuhusu kuonyesha Pepo na Moto kwa picha

Swali: Ni ipi hukumu ya kuchora bustani ambayo inawakilisha Pepo na moto ambao unawakilisha Moto?

Jibu: Haijuzu. Kwa sababu hatutambui namna yavyo. Allaah (´Azza wa Jall) amesema:

فَلَا تَعْلَمُ نَفْسٌ مَّا أُخْفِيَ لَهُم مِّن قُرَّةِ أَعْيُنٍ جَزَاء بِمَا كَانُوا يَعْمَلُونَ

“Hakuna yeyote anayejua yaliyofichiwa katika yanayoburudisha macho yakiwa ni malipo kwa yale waliyokuwa wakiyatenda.”[1]

Hatutambui namna ulivyo Moto. Moto wake umefanywa mbaya zaidi kwa mara sitini na tisa kuliko Myoto ya ulimwenguni kote. Je, yupo yeyote awezaye kuonyesha Moto? Hakuna yeyote awezaye kufanya hivo. Mweleze anayefanya hivo kwamba ni haramu.

Kwa masikitiko makubwa watu hii leo wamekuwa wakiyafanya mambo ya huko Aakhirah kana kwamba ni mambo yenye kuhisiwa na kuonekana. Niliona karatasi imeandikwa vituo mbalimbali kama kifo, kaburi, Qiyaamah na kadhalika. Ni kana kwamba amefikiria yale yanayokuja baada ya kifo ni kama misitari na miraba. Ujasiri wa kipumbavu – ulinzi unaombwa kwa Allaah. Aidha ni kipi kimekujuza kwamba hiki kinakuja baada ya hiki? Tunajua kuwa kaburi linakuwa baada ya kufa na kufufuliwa kunakuwa baada ya kufa, lakini ni nani anayejua upambanuzi kwa mpangilio kama vile hesabu, mizani na kadhalika? Ni ujasiri wa kipumbavu. Jambo la ajabu ni kwamba karatasi hii inatawanywa. Karasi hii ni moja ya vipeperushi vinavyotawanywa kati ya watu ambavo kwa uwongo vinanasibishwa  kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Ni lazima kutahadhari vipeperushi hivi na kuvitahadharisha.

[1] 32:17

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Liqaa’ al-Baab al-Maftuuh (222 B) Tarehe: 1420-08-10/1999-11-18
  • Imechapishwa: 21/09/2021