Ibn ´Uthaymiyn kuhusu kuondosha nywele zilizoko katikati ya paji la uso

Swali: Je, inajuzu kunyoa nywele zilizo kati ya paji la uso ikiwa zimekamatana na pua na zinaufanya uso kuonekana vibaya na khaswa zikiwa ndefu na zenye kudhuru? Mimi naapa kwa Allaah kwamba sijifananisha na mkafiri, mayahudi na kujipamba. Lakini zinauumbua uso wangu.

Jibu: Kuziondosha kwa njia ya kuzichonga ni kitendo cha haramu na hakijuzu. Kwa sababu kufanya hivo ni Nams. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) mwenye kuchonga nyusi na mwenye kuchongwa. Ama kuzindosha bila ya kuzichonga, kama mfano wa kuzikata na kuzinyoa, ni jambo halina neno ingawa wapo baadhi ya wanachuoni wenye kuona kuwa ni haramu na kwamba inaingia katika Nams. Kinachotakikana kwa mwanamke huyu ni kuziacha na wala asizifanye kitu. Isipokuwa zikimdhuru kwa njia ya kwamba kuna kitu katika nywele hizi kinaingia jichoni mwake au zinamzuia kuona vizuri. Katika hali hiyo ni sawa akapunguza zile zinazomdhuru.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Nuur ´alaad-Darb (16) http://binothaimeen.net/content/6808
  • Imechapishwa: 12/03/2021