Ibn ´Uthaymiyn kuhusu kumuadhini na kumkimia mtoto mchanga

Swali: Kuna watu ambao pindi wanaporuzukiwa watoto wanawaadhinia kwenye sikio la upande wa kulia na kuwakimia katika sikio la upande wa kushoto. Je, haya yamethibiti katika Sunnah?

Jibu: Yamethibiti katika Sunnah lakini hata hivyo Hadiyth kuhusu kukimu ni dhaifu. Kuhusu kumtolea adhaana ni zenye nguvu. Kwa ajili hii tunasema mtoto atolewe adhaana kwenye sikio la upande wa kulia pale tu anapozaliwa. Watu wengi hii leo hawawezi kufanya hivi. Kwa sababu watoto wanazalishwa na wauguzi hospitalini. Lakini ikiwa mtu amehudhuria uzalishi basi anatakiwa amuadhinie kwenye sikio lake la kulia. Lakini isiwe kwa sauti ya juu ili asije kulidhuru sikio. Anatakiwa kuadhini kwa sauti ya chini. Wanachuoni wamesema lengo ni kwa sababu kitu cha kwanza ambacho usikizi wake uwe umesikia iwe ni adhaana na wito kwa ajili ya swalah.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Liqaa’ ash-Shahriy (49) http://binothaimeen.net/content/1130
  • Imechapishwa: 13/06/2019