Ibn ´Uthaymiyn kuhusu kula kiapo cha usikivu kwa viongozi wa makundi

Swali: Ni zipi sharti za kiapo cha usikivu na ni ipi hukumu ya kula kiapo kwa mtu asiyetambulika?

Jibu: Ni sharti zipi za kiapo cha usikivu?

Swali: Sharti za kiapo cha usikivu zinakuwepo kwa mfano katika makundi mbalimbali.

Jibu: Viapo vya utiifu vinavyotolewa katika baadhi ya makundi ni dhambi na kitendo kilichopinda. Kitendo hicho maana yake ni kwamba mtu atakuwa juu yake na viongozi na watawala wawili; kiongozi mkuu ambaye anaongoza nchi nzima na kiongozi ambaye amekula kwake kiapo cha usikivu.

Kitendo hicho vilevile kinapelekea katika shari ambayo ni kufanya uasi dhidi ya watawala na matokeo yake yote kama vile kumwagika kwa damu na kuharibika kwa mali.

Kuhusu kundi la wasafiri kuwa na uongozi, hiyo ni Sunnah kuwa na kiongozi wa safari.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Liqaa’ al-Baab al-Maftuuh (6) Sauti: http://www.youtube.com/MuslimerSverige2#p/u/0/s-mGXREKMv0
  • Imechapishwa: 12/07/2021