Ibn ´Uthaymiyn kuhusu Jarh na Ta´diyl


Swali: Je, Jarh na Ta´diyl (kujeruhi na kusifia) imekuja? Ni ipi hukumu ya anayemraddi anayekwenda kinyume pasi na kujali ni nani?

Jibu: Nachelea isije kuwa ni neno la haki ambalo kumekusudiwa batili. Kujeruhi na kusifia hakujafa, hakujazikwa na wala hakujapatwa na ugonjwa na himdi zote njema anastahiki Allaah. Ni jambo bado linaendelea kufnaya kazi.

Kujeruhi na kusifia kunakuwa kwa mashahidi mbele ya hakimu. Wanaweza kumkosoa mpinzani na wanaweza kumuomba hoja.

Kunakuwa pia katika mapokezi. Tumesikia kisomo cha imamu wetu aliposoma:

يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا إِن جَاءَكُمْ فَاسِقٌ بِنَبَإٍ فَتَبَيَّنُوا

“Enyi walioamini! Anapokujieni fasiki kwa habari yoyote, basi pelelezeni.” (49:06)

Kujeruhi na kusifia ni jambo bado linaendelea. Muda wa kuwa watu bado ni wenye kubaki basi kujeruhi na kusifia kunaendelea.

Lakini nachelea mtu akachukua jawabu hili na akalitumua kueneza mapungufu ya mtu na akasema kuwa fulani amejeruhiwa ilihali ukweli wa mambo sio hivyo. Ikiwa mtu ana mapungufu fulani na kuna manufaa, haja au dharurah ya kuyabainisha, basi hapana vibaya kuyabainisha. Hata hivyo bora ni kusema:

“Baadhi ya watu wanafanya au kusema hivi.”

Naonelea hivo kutokana na sababu mbili:

1 – Mtu anaepuka kumlenga mtu.

2 – Hukumu hii inakuwa ni yenye kumgusa yeye na wengine.

Isipokuwa ikiwa tutaona kuwa kuna mtu fulani ambaye watu wamepewa mtihani kupitia yeye na isitoshe analingania katika Bid´ah au upotofu, basi hapo italazimika kumlenga ili watu wasije kughurika naye.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: http://sahab.net/forums/showthread.php?t=376917
  • Imechapishwa: 17/07/2021