Ibn ´Uthaymiyn Kuhusu Ibn Baaz Na al-Albaaniy Na Kuwasengenya Wanachuoni Kama Rabiy´ al-Madkhaliy

Swali: Unaweza kusema kitu juu ya Shaykh Ibn Baaz na Shaykh al-Albaaniy (Rahimahumaa Allaah) waliofariki mwaka uliyopita?

Jibu: Ni katika wanachuoni miongoni mwa wanachuoni wa Ummah wa Kiislamu inapokuja katika Hadiyth, kulingania katika dini ya Allaah na kupambana na Ahl-ul-Bid´ah. Ninachojua kwao ni kuwa ni katika wanachuoni watukufu zaidi kwa uelewa uliyobobea, hata kama mmoja wao ana uelewa uliyobebea zaidi kuliko mwingine. Lakini hata hivyo kuna kheri kw wote wawili.

Swali: Kuna baadhi ya watu wanawasema vibaya wanachuoni waliyoko huko kwenu Saudi Arabia kama mfano wa Shaykh Rabiy´ bin Haadiy na wanachuoni wa al-Madiynah an-Nabawiyyah. Unasemaje juu ya watu hawa wanaosema vibaya wanachuoni wetu?

Jibu: Ni wajibu kwao kufunga vinywa vyao juu ya watu wa kawaida, sembuse juu ya wanachuoni wao. Ikiwa kumsengenya mtu wa kawaida ni katika madhambi makubwa, basi kumsengenya mwanachuoni ni dhambi kubwa zaidi na zaidi. Kwa sababu kumsengenya mwanachuoni hakufupiki na kule mtu wa kawaida kumdharau tu, bali kunapelekea kuachwa kwa maoni yake anayosema juu ya Shari´ah ya Allaah. Matokeo yake watu wanayadharau maneno yake yaliyojengwa juu ya Shari´ah ya Allaah.

Kuwasengenya wanachuoni ni khatari na dhambi kubwa inayopelekea katika adhabu kubwa. Ni juu ya watu hawa kufunga vinywa vyao juu ya kuwatukana wanachuoni na kuwaponda na vilevile waseme neno la haki juu ya maoni na sio juu ya wanaume.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: http://www.sahab.net/forums/index.php?showtopic=143368
  • Imechapishwa: 15/01/2017