Ibn ´Uthaymiyn kufumba macho katika swalah kwa ajili ya unyenyekevu

Swal: Ni ipi hukumu ya kufumba macho katika swalah kwa ajili ya kutafuta unyenyekevu? Nimesikia kwamba Ibn-ul-Qayyim anaona kuwa ni jambo linalofaa na huenda likawa lenye kupendekeza kwa ajili ya unyenyekevu?

Jibu: Ikiwa kuna mambo yanayompelekea kufanya hivo hakuna neno. Kwa mfano punde tu alipoingia ndani ya swalah wakaanza kupita mbele yake watoto na kuanza kucheza au akaona kitu chenye kumshughulisha kutokamana na swalah, katika hali hii ni sawa akafumba macho. Ama kufanya hivo pasi na sababu na akaona kuwa akifumba ndio anakuwa ni mnyenyekevu, hii ni njia ya shaytwaan. Kwa sababu kufumba macho katika swalah ni jambo limechukizwa. Imesemekana kuwa ni kitendo cha waabudu moto wakati wanapoabudu kwao moto.

Kwa hivyo kufumba macho ni jambo linalohitajia maelezo. Ikiwa ni kwa jambo lililotokea na ukachelea macho yake yasilikodolee na likakushughulisha kutokamana na swalah yako, hapa unaweza kufumba macho yako. Ama kusema unafumba macho yako kwa ajili ya kutafuta unyenyekevu ni makosa.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Liqaa’ ash-Shahriy (40) http://binothaimeen.net/content/898
  • Imechapishwa: 22/08/2018