Ibn ´Uthaymiyn kisomo cha Taraawiyh

Swali: Kuna kidhibiti gani kwa kiwango cha kisomo kwenye kila Rak´ah katika Taraawiyh? Je, inatosha kwa imamu kusoma nusu ya Qur-aan kwa mwezi au theluthi yake?

Jibu: Ikiwa watu wamefungwa na mambo, basi itategemea vile wapendavyo. Wakitaka watarefusha na wakitaka watafupisha. Ama wakiwa hawakufungwa na mambo, basi haitakiwi kurefusha kusomo. Sio lazima kukamilisha Qur-aan. Usiwarefushie ukawachokesha. Lakini kitu muhimu zaidi ni Rukuu´, Sujuud, kuinuka kutoka katika Rukuu´, kukaa kati ya sijda mbili na Tashahhud. Kwa masikitiko wengi ambao wanaswali Taraawiyh wanapofikia:

أشهد أن لا إله إلا الله وأشهد أن محمداً عبده ورسوله، اللهم صل على محمد

“Nashuhudia ya kwamba hapana mungu wa haki isipokuwa Allaah na kwamba Muhammad ni mja na Mtume wake. Ee Allaah! Mswalie Muhammad… “

kisha wanatoa salamu. Hili ni kosa. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Ataposoma mmoja wenu Tashahhud ya mwisho basi aseme:

اللهم إني أعوذ بك من عذاب جهنم، ومن عذاب القبر، ومن فتنة المحيا والممات، ومن فتنة المسيح الدجال

“Ee Allaah! Hakika mimi najilinda Kwako kutokamana na adhabu ya Moto, adhabu ya kaburi, fitina ya uhai na ya kifo na fitina ya al-Masiyh ad-Dajjaal.”

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Liqaa’ ash-Shahriy (52) http://binothaimeen.net/content/1183
  • Imechapishwa: 10/07/2019