Ibn ´Uthaymiyn idadi ya Takbiyr za ´Iyd


Swali: Kuna Takbiyr ngapi katika swalah ya ´Iyd?

Jibu: Idadi ya Takbiyr katika swalah ya ´Iyd ni jambo lina tofauti. Wametofautiana kwalo wanachuoni wa kale na wa sasa. Katika Rakaa´ ya kwanza mwenye kutoa Takbiyr saba na kwenye Rakaa´ ya pili baada ya kusimama akatoa Takbiyr tano ni vizuri. Ni vizuri pia akifanya kinyume na hivo kwa sababu imethibiti kutoka kwa Salaf.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawa (16/238)
  • Imechapishwa: 14/06/2018