Ibn ´Uthaymiyn anakemea Niqaab na Burqu´ za kiujanja

Swali: Unasemaje juu ya wanawake kuvaa Burqu´ pamoja na kujiachia huku ambako kunapatikana hii leo?

Jibu: Mimi najizuia kufutu hilo. Naona kuwa mwanamke asiivae. Kwa sababu ni fitina. Wako baadhi ya wanawake ambao wanachukulia wepesi. Wanafungua sehemu kubwa ya macho kwa kiasi cha kwamba macho yanaonekana. Baadhi ya wengine wanaonyesha macho hali ya kuwa wamejipaka wanjaMatokeo yake anajiweka katika mtihani. Naona kuwa mwanamke abaki kama alivyokuwa hapo kabla. Afunike uso wake kikamilifu kama anavyofunika kichwa chake.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Liqaa’ ash-Shahriy (56) http://binothaimeen.net/content/1289
  • Imechapishwa: 12/10/2019