Swali: Inajuzu kwa mwanamke kuvaa Hijaab nyeupe, kijani au rangi nyenginezo ikiwa hii ndio desturi kwa watu wake na khaswa ikiwa baadhi ya wanawake wajinga wanamuona ni kituko pindi anapovaa Jilbaab nyeusi?

Jibu: Hakuna neno ikiwa hii ni desturi ya nchi akavaa vazi leupe. Lakini hata hivyo isiwe katika shakili ya mavazi ya wanaume. Katika hali hii hakuna neno. Rangi haizingatiwi. Kwa sharti nguo yake ipambanuke na nguo ya mwanaume. Ama ikiwa sio katika desturi za watu wa mji wake, basi lililo la wajibu ni yeye kufuata desturi za watu wa mji wake. Avae vazi leusi, kijani au jekudu kwa kutegemea ada. Anachotakiwa ni yeye kufunika uso wake wote.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Liqaa´ ash-Shahriy (66) http://binothaimeen.net/content/1488
  • Imechapishwa: 26/01/2020