Ibn-ul-Qayyim kuhusu kuanza kusoma Suurah katikati yake wakati wa swalah

Swali: Wakati fulani Imamu wa Msikiti wetu katika Swalah ya al-Fajr Rakaa ya kwanza anasoma kuanzia katikati ya Suurat-ul-Baqarah na katika Rakaa ya pili anasoma mwisho wa Suurah. Je, kitendo chake hichi ni sahihi?

Jibu: Ni sahihi. Kuhusu usahihi ni sahihi. Lakini Ibn-ul-Qayyim (Rahimahu Allaah) anasema mtu asianze kusoma katikati ya Suurah au mwisho wake. Aanze Suurah kuanzia mwanzo wake na asome kiasi cha atakavyoweza. Ni bora kuliko kuikatakata Suurah na kuanza katikati yake au mwisho wake

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Zaad-il-Ma´aad (72) http://www.alfawzan.af.org.sa/node/14085
  • Imechapishwa: 17/11/2014