Imaam Ibn-ul-Qayyim (Rahimahu Allaah) amesema:

Sura: Dalili ya tatu ni maneno Yake (Ta´ala):

وَاللَّـهُ يَدْعُو إِلَىٰ دَارِ السَّلَامِ وَيَهْدِي مَن يَشَاءُ إِلَىٰ صِرَاطٍ مُّسْتَقِيمٍ لِّلَّذِينَ أَحْسَنُوا الْحُسْنَىٰ وَزِيَادَةٌ ۖ وَلَا يَرْهَقُ وُجُوهَهُمْ قَتَرٌ وَلَا ذِلَّةٌ ۚ أُولَـٰئِكَ أَصْحَابُ الْجَنَّةِ ۖ هُمْ فِيهَا خَالِدُونَ

“Allaah anaitia katika nyumba ya amani na anamwongoza amtakaye kuelekea njia iliyonyooka. Kwa wale waliofanya mazuri watapata wema na zaidi na wala vumbi halitowafunika nyuso zao na wala [hawatopatikana na] udhalilifu. Hao ni watu wa Peponi. Wao humo ni wenye kudumu.” (10:25-26)

“Wema” ni Pepo. “zaidi” ni kuona Uso Wake Mtukufu. Hivyo ndivyo alivyofasiri Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ambaye ndiye ambaye ameteremshiwa Qur-aan na Maswahabah baada yake.

  • Mhusika: ´Allaamah Rabiy´ bin Haadiy al-Madkhaliy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Bayaan wa al-Idhwaah li ´Aqiydah Ahl-is-Sunnah wal-Jamaa´ah fiy Ru´yati Allaahi yaum al-Qiyaamah, uk. 27
  • Imechapishwa: 27/08/2020