Ibn Taymiyyah anaona kufaa kuliendea kaburi na kuliomba?

Swali: Mwenye kwenda kwenye kaburi na akamuomba mtu yule amuombee kwa Allaah.

Jibu: Hii ni shirki pia. Kwa sababu maiti hamiliki jambo hilo. Akimwambia “nifanyia uombezi” au “niombee kwa Allaah” basi amemshirikisha Allaah kwa mujibu wa maoni sahihi. Kwani amemuomba kitu asichokiweza.

Swali: Wako wanaodai kwamba haya ni maoni ya Ibn Taymiyyah. Je, ni sahihi?

Jibu: Hapana, hayakusihi kutoka kwa Ibn Taymiyyah. Ibn Taymiyyah amesema wazi kwamba kitendo hichi ni shirki kubwa.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Kashf-ish-Shubuhaat, uk. 57
  • Imechapishwa: 28/06/2019