Ibn Taymiyyah amejuzisha Subha, lakini sisi tunawafata Salaf

Je, Salaf, baada ya kuzuka Subha, walikuwa wakiingiza mikono yao mifukoni mwao na kuzitoa baada ya kumalizika kuswali na wakiketi na kusoma Dhikr kwa kuzitumia? Au walikuwa wakifanya Dhikr kwa vidole vyao? Hapana shaka kwamba hilo la pili ndilo walikuwa wakifanya. Shubha ni Bid´ah ni miongoni mwa Bid´ah za Suufiyyah. Hilo tu linatosha. Pamoja na kwamba Bid´ah hii inakwenda kinyume na Sunnah, hatuoni kuwa Ibn Taymiyyah (au wengineo ambao wameafikiana naye) amepatia katika kuijuzisha. Yale ambayo Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ametubainishia yanatutosha;  amefanya hivo kimaneno na kivitendo kwa kuonyesha kwamba Dhikr inatakiwa kufanywa kwa kutumia vidole vya mkono wa kulia.

Mpaka hii leo tunaona namna ambavyo waislamu wa zamani wanajifananisha na manaswara kwa kutumia Subha hizi. Subha msingi wake ni kutoka kwa manaswara[1] zikaenda kwa waislamu. Manaswara wamezichukua kutoka kwa mabudha[2]. Kwa hivyo ni uzushi wa tangu kale kutoka kwa baadhi ya wafuasi wa dini kabla ya Uislamu. Ikaingia kwa manaswara na wakazusha kama walivyozusha utawa na mengineyo. Kisha baada ya hapo ikatoka kwa manaswara na kwenda kwa waislamu. Kwa ajili hiyo sisi hatuoni kuwa inafaa kuhesabu kwa kutumia Subha kwa sababu inapingana na Sunnah ambayo ni Swahiyh.

[1] Tazama https://vatican.com/2/Rosaries-Faceted-Glass

[2] Tazama https://www.amazon.com/Hztyyier-Tibetan-Necklace-Buddhist-Bracelet/dp/B07Y3BG42N

  • Mhusika: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa Juddah (33) Tarehe: 1.06.29
  • Imechapishwa: 11/06/2021