Zipo Hadiyth ambazo ni Swahiyh. Zipo nyenginezo ambazo si Swahiyh. Huu ndio mgawanyo wa kwanza. Baadaye kukaja mgawanyo wa Swahiyh, nzuri, dhaifu na Hadiyth zilizozuliwa, sembuse mgawanyo mwingine. Ndio maana wanasema kuwa Imaam at-Tirmidhiy ndiye ambaye alizigawanya kwenda Swahiyh na nzuri na kueneza mpangilio huo. Hili linashuhudiwa na uhalisia. Alipokea mgawanyo huo kutoka kwa Imaam al-Bukhaariy. Lakini at-Tirmidhiy ndiye ambaye aliutumia kwa bidii.

Hii ina maana kwamba Imaam Ahmad, ambaye ndiye mwalimu wa waalimu, mwalimu wa al-Bukhaariy, istilahi ya “Swahiyh” na “nzuri” haikuwa yenye kuzoeleka kwake. Kwake alikuwa na Swahiyh na dhaifu peke yake. Wakati aliposema kuwa anaipa kipaumbele Hadiyth dhaifu mbele ya kipimo (Qiyaas), alikuwa anakusudia nzuri na si dhaifu kwa maana iliozoeleka na wale waliokuja nyuma. Maneno haya yamepambanuliwa na Shaykh-ul-Islaam (Rahimahu Allaah). Ameitumikia elimu kiasi kikubwa.

Msikilizaji: Bwana huyu alikuwa wa ajabu.

al-Albaaniy: Alikuwa ni ummah, ummah.

Msikilizaji: Baadhi wamesema kuwa yeye mwenyewe hajapatapo kuona mfano wake.

al-Albaaniy: Kiukweli ni kwamba haya yanasemwa kwa wanazuoni na watu wabora wengi, lakini mara ndani yake kuna kuongeza chumvi. Lakini Ibn Taymiyyah kiukweli alikuwa kama ile methali ya kisyria inayosema:

“Alikuwa kama sahani la kichina; vovyote utakavyolitupa basi linapiga ukelele.”

Elimu yoyote anayoingia ndani… Mpaka wakamtolea ushuhuda. Anapoketi na wanazuoni na akazungumza, basi anazungumza kwa njia inayowafanya kumdhania kwamba ni mtaalamu wa mada hiyo. Hapa hakuna kuongeza chumvi. Ni maneno ya kihakika.

Suufiyyah huwa wanasema kuwa mawalii wao wanamtambua Allaah. Mimi naonelea kwamba wasifu huu unatumika kwa Ibn Taymiyyah. Utamsikia anayasema mambo ambayo hutoyapata kwengine. Kwa kweli alikuwa amejaaliwa. Utawaona wanazuoni wengine wamesoma na kuketi sana chini ya wanazuoni, lakini hakuna wanachofanya isipokuwa kunukuu peke yake. Hawaji na jipya kwa mazingira mazuri. Lakini Ibn Taymiyyah ni mambo mengine…

  • Mhusika: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Silsilat-ul-Hudaa wan-Nuur (548) Dakika: 56:45
  • Imechapishwa: 22/06/2021