Ibn Baaz kutumia vidonge vya kuzuia hedhi kwa ajili ya Ramadhaan


Swali: Je, inajuzu kwa mwanamke kutumia vidonge vya kuzuia mimba kwa ajili ya kuchelewesha hedhi katika mwezi wa Ramadhaan?

Jibu: Hakuna neno juu ya hilo kutokana na yale manufaa yanayopatikana kwa mwanamke katika kufunga kwake pamoja na wengine na kutolipa baadaye. Hata hivyo inatakiwa kuchunga asije kudhurika. Kwa sababu baadhi ya wanawake vidonge vinawadhuru.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (15/201)
  • Imechapishwa: 23/05/2018