Ibn Baaz kuthibiti na kuisha kwa Ramadhaan

Swali: Ni kwa kitu gani kunathibiti kuingia kwa mwezi na kuisha kwake? Ni ipi hukumu kwa yule ambaye ameuona mwezi peke yake wakati wa kuingia kwa Ramadhaan au kuisha kwake?

Jibu: Kunathibiti kuingia kwa Ramadhaan na kuisha kwake kwa kuuona mwezi mtu mmoja mwadilifu au zaidi ya mmoja. Kuingia kwake kunathibiti kwa kuuona mwezi mtu mmoja tu. Kwa sababu imethibiti ya kwamba Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Wakishuhudia mashahidi wawili, basi fungeni na fungueni.”[1]

Vilevile imethibiti kwake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kwamba aliwaamrisha watu wafunge kwa mwezi kuonekana na Ibn ´Umar (Radhiya Allaahu ´anhumaa) na mbedui mmoja. Hakuwataka (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) mashahidi wengine. Hekima ya hilo – na Allaah ndiye mjuzi zaidi – ni ule usalama katika dini katika kuingia kwake na kuisha kwake, kama walivyosema wanawachuoni.

Yule ambaye atauona mwezi peke yake wakati wa kuingia kwake Ramadhaan  na asitendee kazi ushahidi wake, basi anatakiwa kufunga na kufungua pamoja na watu. Si lazima kwake kutendea kazi ushahidi wake mwenyewe kwa mujibu wa maoni ya wanachuoni ambayo ni sahihi zaidi. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Fungeni siku mnafunga, fungueni siku mnafungua na chinjeni siku mnachinja.”[2]

[1] Ahmad (18416) na an-Nasaa´iy (2116).

[2] at-Tirmidhiy (697).

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (15/63)
  • Imechapishwa: 15/05/2018