Ibn Baaz kusema kwamba Mtume ni tiba na dawa ya mioyo


Swali: Ni ipi hukumu ya mwenye kusema ndani ya swalah kuhusu Mtume:

اللهم صل على محمد طبّ القلوب و دوائها

“Ee Allaah! Mswalie Muhammad ambaye ni tiba na dawa ya mioyo”?

Jibu: Maneno haya si sahihi. Ni maneno ya kijumla. Kusema kwamba ni tiba na dawa ya mioyo ni maneno ya kijumla. Tiba na dawa ya mioyo ni kwa kufuata Shari´ah. Haya yanaweza kumfanya mtu akaelewa kwamba yeye ndiye anatibu na ni dawa kwa nafsi yake mwenyewe na kwamba ananufaisha na anadhuru. Maneno haya si sahihi. Wafunzeni watu matamshi sahihi:

اللهم صل على محمد و على آل محمد كما صليت على آل إبراهيم

“Ee Allaah! Msifu Muhammad na jamaa zake Muhammad kama Ulivyomsifu Ibraahiym… ”

Au:

اللهم صل على النبي الأمي

“Ee Allaah! Msifu Mtume ambaye si msomi…”

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Kashf-ish-Shubuhaat, uk. 49
  • Imechapishwa: 20/06/2019