Ibn Baaz kujiunga na imamu katika Tarawiyh kwa nia ya ´Ishaa


Swali: Tunaona katika baadhi ya misikiti wale ambao wanakuja baada kumalizika swalah ya ´Ishaa na mwanzoni mwa Tarawiyh wanasimamisha swalah ya pili. Kitendo chao hichi wanawashawishi wale wanaoswali Tarawiyh. Je, lililo bora kwao ni wao kuanza swalah ya mkusanyiko wa pili au wajiunge pamoja na imamu katika Tarawiyh kwa nia ya kuswali ´Ishaa? Je, hukumu inatofautiana ikiwa yule aliyeingia ni mtu mmoja au ni kundi la watu?

Jibu: Ikiwa wale walioingia sio chini ya watu wawili lililo bora kwao ni wao kuswali swalah ya ´Ishaa kivyao kisha ndio wajiunge pamoja na wengine katika Tarawiyh. Vilevile hapana neno endapo watajiunga pamoja na imamu kwa nia ya kuswali ´Ishaa. Pale ambapo imamu atatoa salamu basi kila mmoja atakamilisha kivyake. Kwa sababu imethibiti ya kwamba Mu´aadh (Radhiya Allaahu ´anh) alikuwa akiswali pamoja na Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) swalah ya ´Ishaa faradhi, kisha anarudi kwa watu wake na anawaswalisha swalah hiyo hiyo. Swalah hiyo kwake inakuwa ni sunnah na kwa wao maimamu inakuwa ni faradhi[1].

Ama yule mwenye kuingia msikitini akiwa ni mmoja lililo bora kwake ni yeye kujiunga pamoja na imamu kwa nia ya kuswali ´Ishaa ili aweze kupata fadhilah za kuswali mkusanyiko. Imamu akitoa Tasliym baada ya Rakaa´ mbili asimame na kukamilisha kivyake swalah ya ´Ishaa.

[1] al-Bukhaariy (6106), Muslim (583) na wengineo.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (30/29-30)
  • Imechapishwa: 03/06/2018