Swali: Ambaye hajui kuwa kuchinja ni ´ibaadah na kwamba kuweka nadhiri ni ´ibaadah. Ni ipi hukumu yake?

Jibu: Mjinga afunzwe. Mjinga afunzwe.

Swali: Je, asihukumiwe shirki?

Jibu: Anahukumiwa ukafiri na afunzwe. Yeye hakusikia Allaah akisema:

أَمْ تَحْسَبُ أَنَّ أَكْثَرَهُمْ يَسْمَعُونَ أَوْ يَعْقِلُونَ

“Je, unadhania kwamba wengi wao wanasikia au wanatia akilini?”[1]

Wanyama wanafahamu:

إِنْ هُمْ إِلَّا كَالْأَنْعَامِ ۖ بَلْ هُمْ أَضَلُّ سَبِيلًا

“Si vyenginevyo isipokuwa ni kama wanyama, bali wao wamepotea zaidi njia.”[2]

Vilevile amesema (Jalla wa ´Alaa):

وَلَقَدْ ذَرَأْنَا لِجَهَنَّمَ كَثِيرًا مِّنَ الْجِنِّ وَالْإِنسِ ۖ لَهُمْ قُلُوبٌ لَّا يَفْقَهُونَ بِهَا وَلَهُمْ أَعْيُنٌ لَّا يُبْصِرُونَ بِهَا وَلَهُمْ آذَانٌ لَّا يَسْمَعُونَ بِهَا ۚ أُولَـٰئِكَ كَالْأَنْعَامِ بَلْ هُمْ أَضَلُّ ۚ أُولَـٰئِكَ هُمُ الْغَافِلُونَ

“Hakika Tumeumba Moto wa Jahannam kwa ajili ya wengi katika majini na watu – wana nyoyo, lakini hawafahamu kwazo na wana macho, lakini hawaoni kwayo na wana masikio, lakini hawasikii kwayo – hao ni kama wanyama, bali wao ni wapotovu zaidi. Hao ndio walioghafilika.”[3]

[1] 25:44

[2] 25:44

[3] 07:179

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Kashf-ish-Shubuhaat, uk. 42
  • Imechapishwa: 17/06/2019