Ibn Baaz kuhusu ujinga ni udhuru VII

Swali: Mtunzi (Rahimahu Allaah) amesema:

“Huenda akalisema na yeye ni mjinga, hata hivyo hapewi udhuru.”

Jibu: Kwa sababu anaishi kati ya waislamu, karibu naye yuko na Qur-aan na Sunnah. Kwa msemo mwingine huyu anachukulia wepesi.

Swali: Haya yanafasiriwa kwamba ni yule mtu ambaye ni mzembe?

Jibu: Ndio. Ni mtu mzembe ambaye anaweza kujifunza lakini hata hivyo hakujali.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Kashf-ish-Shubuhaat, uk. 26
  • Imechapishwa: 08/06/2019