Swali: Ni ipi hukumu ya kutumia ugoro unaowekwa mdomoni? Tunaomba uwatumie fatwa misikiti ya mkoa wa kusini Jiyzaan kwa sababu umeenea katika mkoa huo na kwa kutarajia wahusika watalishughulikia suala hilo kwa sababu unauzwa katika masoko ya mkoa huo mbele za watu.

Jibu: Aina zote za sigara ni haramu, chafu na ni zenye kudhuru. Ni mamoja ugoro au kitu kingine. Ni lazima kwa mwenye busara kujiepusha na jambo hilo. Balaa hili limekusanya madhara ya dini, ya mwili na ya mali. Ni miongoni mwa vichafu vya haramu. Pamoja na hayo unadhuru mwili wa mtu na afya yake, unadhuru mali yake na uchumi wake, unaidhuru dini yake kwa sababu ya uchafu wake na uharamu wake.

Kwa hivyo ni lazima kwa mwenye kuutumia kuutahadhari. Haijuzu kuufanyisha biashara; kuuza na kuununua ni haramu. Kadhalika kupeana zawadi. Vivyo hivyo kuutumia. Kama ambavo pombe ni haramu kwa aina zake zote vivyo hivyo aina mbalimbali za sigara kutokana na madhara mengi yanayopatikana ndani yake na uchafu mkubwa.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/3410/%D8%AD%D9%83%D9%85-%D8%A7%D8%B3%D8%AA%D8%B9%D9%85%D8%A7%D9%84-%D8%A7%D9%84%D8%B4%D9%85%D8%A9
  • Imechapishwa: 25/10/2019