Swali: Ni ipi hukumu ya swawm ya ambaye haswali isipokuwa tu katika Ramadhaan? Bali huenda akafunga na huku haswali?

Jibu: Kila ambaye amehukumiwa ukafiri basi matendo yake yote ni yenye kubatilika. Amesema (Ta´ala):

وَلَوْ أَشْرَكُوا لَحَبِطَ عَنْهُم مَّا كَانُوا يَعْمَلُونَ

“kama wangemshirikisha, bila shaka yangeliharibika yale yote waliyokuwa wakitenda.” (06:88)

وَمَن يَكْفُرْ بِالْإِيمَانِ فَقَدْ حَبِطَ عَمَلُهُ وَهُوَ فِي الْآخِرَةِ مِنَ الْخَاسِرِينَ

“Yeyote mwenye kukanusha imani, basi hakika yameharibika matendo yake – naye Aakhirah atakuwa miongoni mwa waliokhasirika.” (05:05)

Wapo wanachuoni ambao wanaonelea kuwa hakufuru ukafiri mkubwa midhali ni mwenye kukubali uwajibu kwake. Lakini hata hivyo wanaonelea kuwa ukafiri wake ni mdogo na kitendo chake hichi kinakuwa kibaya zaidi kuliko kitendo cha mzinzi, mwizi na mfano wa hayo. Pamoja na haya yote wao wanaonelea kuwa swawm na hajj yake vinahisi maadamu atayatekeleza kwa njia iliyowekwa katika Shari´ah. Lakini jinai yake itakuwa ni kule kutohifadhi swalah. Hata hivyo yuko katika khatari kubwa ya kutumbukia katika shirki kubwa kwa mtazamo wa kundi la wanachuoni. Kuna ambao wamesimulia mtazamo wa wengi ambao wanasema kuwa hakufuru ukafiri mkubwa endapo ataiacha kwa kuzembea na kwa uvivu. Bali wanaona kuwa amekufuru ukafiri mdogo, amefanya dhambi kubwa na maovu yanayotia kinyaa yaliyo makubwa zaidi kuliko uzinifu, kuiba na utovu wa nidhamu kwa wazazi wawili. Wanaona kuwa dhambi hiyo ni kubwa zaidi kuliko kunywa pombe – tunamuomba Allaah usalama.

Lakini maoni ya wanachuoni yaliyo ya sawa na sahihi ni kwamba anakufuru ukafiri mkubwa kutokana na zile dalili za Kishari´ah. Kwa hiyo mwenye kufunga na akawa haswali, swawm na hajj yake si sahihi.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (15/179-180)
  • Imechapishwa: 16/05/2018