Ibn Baaz kuhusu mwanamke kupanda gari peke yake na dereva wa kiume

Swali: Ni ipi hukumu ya mwanamke kupanda gari pamoja na derava wa kando akiwa peke yake kwa ajili ya kutatua haja za familia yake? Mume wake ni mzee na watoto wake wameshughulishwa na masomo au kwa ajili ya maisha yao maalum. Anatembelea na dereva huyu ndani ya mji na anaweza kutoka nje kidogo kwenda kitongoji kilicho karibu na mji huo takriban kilomita 10. Naomba uniwekee wazi hukumu.

Jibu: Haijuzu kwa mwanamke kutoka pamoja na dereva; si ndani ya mji wala katika kitongoji cha nje kidogo. Kwa sababu hii ni chemba ambayo imeharamishwa. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Mwanaume asikae chemba na mwanamke. Kwani shaytwaan ndiye watatu wao.”

“Mwanaume asikae chemba na mwanamke isipokuwa awe pamoja naye Mahram.”

Kwa hivyo haijuzu kwake kwenda pamoja na dereva. Kwa sababu ndani yake kuna khatari kubwa. Pengine dereva huyo akamfanyia usaliti, pengine akafanya maovu. Tunachokusudia ni kwamba haijuzu hata kama dereva huyo ni miongoni mwa watu bora na watu wema. Haijuzu kwake mwanamke huyo kwenda pamoja naye akiwa peke yake. Ni lazima aambatane na mtu wa tatu ima mke wa dereva huyo, mama yake, dada yake au mmoja katika majirani zake. Ni lazima wawe na mtu wa tatu. Kwa sababu katika hali hiyo shaytwaan hatokuwa watatu wao. Wakiwa na mtu watatu basi shaytwaan hatokuwa watatu wao. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Mwanaume asikae chemba na mwanamke. Kwani shaytwaan ndiye watatu wao.”

Bi maana atawapambia machafu. Kwa hivyo ni lazima kuchukua tahadhari na kamwe mwanamke asitoke isipokuwa awe na mtu watatu au mtu wanne. Haijalishi kitu ijapokuwa haja zake zitaharibika. Haifai kamwe akatoka na dereva. Si kutoka kwenda masomoni, mahakamani, sokoni wala kwengineko. Yote haya ni dhambi na ndani yake kuna khatari kubwa. Tunamuomba Allaah atuongoze sote na atusalimishe.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/10424/حكم-ركوب-المراة-مع-ساىق-اجنبي
  • Imechapishwa: 21/12/2019