Ibn Baaz kuhusu mwanamke kupanda gari peke yake na dereva wa kiume II

Swali: Je, inafaa kwa mwanamke kupanda gari pamoja na dereva peke yake au pamoja na mtoto wa kiume mdogo? Je, inafaa kwa mwanamke kusafiri na ndege peke yake pasi na Mahram?

Jibu: Hili limebainishwa mra nyingi katika “Nuur ´alaad-Darb” na katika gazeti la “ad-Da´wah”. Haijuzu. Kwa mnasaba napenda kuzindua kwamba katika gazeti la “ad-Da´wah” kuna makala na majibu yenye faida. Anatakiwa kurejea huko yule anayetaka faida. Kwa kifupi ni kwamba haifai kwa mwanamke kupanda gari peke yake pamoja na dereva wa kiume akiwa mwanamme huyo ni wa kando naye na si Mahram wake. Ni lazima awepo mtu wa tatu kama vile kaka yake, mama yake, shangazi yake na mfano wake. Lengo ni kuondokane ile chemba. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Mwanamme asikae chemba na mwanamke. Kwani hakika shaytwaan ndiye watatu wao.”

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/4352/حكم-سفر-المراة-وحدها-وركوبها-مع-الساىق
  • Imechapishwa: 17/06/2022