Swali: Inajuzu kusema ifuatavyo:

“Allaah na Mtume Wake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ndio wamekingwa na kukosea?”

Jibu: Ndio, ni sawa. Allaah hasemi na wala hafanyi makosa. Kila anachokisema ni haki, sifa Zake zote ni haki na matendo yake yote ni haki.

Kuhusiana na Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amekingwa na kukosea katika yale anayofikisha kutoka kwa Allaah. Mitume wote (´alayhimus-Salaam) wamekingwa na kukosea kwa njia ya kwamba hawawezi kumsemea uongo Allaah na hawawezi kukosea kwa yale anayowapa Allaah [kufikisha kwa watu].

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh al-´Aqiydah al-Waasitwiyyah (01)
  • Imechapishwa: 09/08/2020