Hapo kabla nilikuwa nikichukua msimamo wa kunyamaza kuhusiana na mawaidha na semina ya video. Nilikuwa nikikereka na jambo hilo na sikuwa mwenye kuridhia mihadara kuchukuliwa video. Muda ulivokuwa unaenda nikaona kuwa zinanufaisha jamii ya waislamu ili waweze kunufaika na makongamano na mihadhara inayorushwa kupitia njia ya runinga. Kwa sababu ikiwa picha za vitambulisho zinafaa kwa sababu zina manufaa na ni haja kwa mtu mmojammoja, tusemeje juu ya kitu ambacho manufaa yake ni yenye kuwaenea watu wote. Kwa ajili hiyo sitilii mkazo sana juu ya kukataza kuchukua video makongamano na mihadhara ambayo manufaa yake yanawaenea waislamu wote. Hapana shaka kwamba maoni yanayokataza pia yana mtazamo fulani, lakini kwa hivi sasa naona kuwa kile kitu chenye manufaa yenye kuwaenea watu wote kwa jumla ni chenye nguvu zaidi kuliko kile chenye manufaa kwa mtu mmojammoja.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://youtu.be/gVQKYAPLwHc
  • Imechapishwa: 17/05/2021