Ibn Baaz kuhusu mahali pa mikono baada ya Rukuu´

Swali: Ni wapi waswaliji wanatakiwa kuiweka mikono yake baada ya Rukuu’?

Jibu: Sunnah ni kuiweka mikono miwili juu ya kifua. Ni mamoja kabla na baada ya swalah. Amesema (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) katika Hadiyth Swahiyh katika yake yaliyopokelewa na Muslim katika “as-Swahiyh” yake kutoka kwa Waa-il ambaye amesema:

“Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alikuwa akiweka mkono wake wa kuume juu ya kitanga chake cha kushoto.”

Sahl bin Sa´d (Radhiya Allaahu ´anh) amesema:

“Mtu alikuwa akiamrishwa kuweka mkono wake wa kuume juu ya dhiraa yake ya kushoto ndani ya swalah.”

Katika “al-Musnad” ya Imaam Ahmad na wengineo kutoka kwa Swahabah mmoja aliyesema:

“Alimuona Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akiweka mikono yake juu ya kifua chake ndani ya swalah.”

Waa-il amesema:

“Nilimuona Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akiweka mikono yake juu ya kifua chake ndani ya swalah.”

Hii ndio Sunnah. Anatakiwa kuiweka juu ya kifua chake wakati wa kusimama ndani ya swalah. Ni mamoja kabla na baada ya Rukuu´. Hakuna tofauti katika hilo. Kwa sababu Waa-il amesema:

“Nilimuona Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) anapokuwa amesimama ndani ya swalah basi huweka mkono wake wa kuume juu ya mkono wake wa kushoto juu ya kifua chake ndani ya swalah.”

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/2814/%D8%A7%D9%8A%D9%86-%D9%8A%D8%B6%D8%B9-%D8%A7%D9%84%D9%85%D8%B5%D9%84%D9%8A-%D9%8A%D8%AF%D9%8A%D9%87-%D8%A8%D8%B9%D8%AF-%D8%A7%D9%84%D8%B1%D9%83%D9%88%D8%B9
  • Imechapishwa: 10/01/2020