Ibn Baaz kuhusu kutoa Zakaat-ul-Fitwr na kuituma nje ya nchi


Swali: Inajuzu kutoa Zakaat-ul-Fitwr pesa? Inajuzu kuitoa nje ya nchi ya mtu?

Jibu: Wanachuoni wengi wanaonelea kuwa haijuzu kuitoa kwa aina ya pesa. Ni wajibu kutoa chakula. Hivyo ndivo alivofanya Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na Maswahabah (Radhiya Allaahu ´anhum). Ni pishi moja katika chakula cha mji. Kama mfano wa tende, mchele na vyenginevyo kwa pishi ya Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Anatakiwa kutoa mvulana, msichana, mdogo, mkubwa, muungwana na mtumwa muislamu.

Sunnah ni mtu aitoe kati ya mafukara wa nchi ya yule anayetoa na asiiagize katika nchi nyingine. Lengo ni mtu awatajirishe mafukara wa mji na kuziba mahitajio yao. Inajuzu kuitoa siku moja au mbili kabla ya ´Iyd. Hivo ndivo walivokuwa wakifanya Maswahabah wa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na (Radhiya Allaahu ´anhum). Katika hali hiyo wakati wake unakuwa ni wenye kuanza tokea ule usiku wa tarehe ishirini na nane Ramadhaan.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (14/213)
  • Imechapishwa: 12/06/2018